Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha ndug.Thomas Ole Sabaya ameendelea na ziara yake yakukagua miradi ya maendeleo pamoja nakusikiliza na kutatua kero za wananchi wilayani Monduli ikiwa ni kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.(CCM)
Ambapo katika ziara yake katika kata ya Lolkisale iliyofanyika jana amekagua jengo la zahanati ya NAFCO sambaba na hilo amepongeza jitihada zilizofanyika kwa ujenzi wa jengo hilo nakusema kazi iliyofanyika ni nzuri kwa kutizama na kuridhisha.
"Nakupongeza Mganga mkuu wa wilaya kwakusimamia ujenzi wa zahanati ya NAFCO mpaka kumalizika wananchi wanapata huduma nzuri Sasa"amesema Sabaya.
Breath Browden ni Daktari anaetoa huduma kwa wagojwa zahanati ya NAFCO amesema mpaka Sasa changamoto kubwa inayowakabili ni kujengewa fensi/uzio katika hospitali ili kuzuia wanyama wakali nyakati za usiku kuweza kuvamia mbali na hilo baadhi ya wagojwa wanaolazwa kutoroka nyakati za usiku.ombi lingine lililowekwa wazi na Daktari Breath ni ujenzi wa nyumba za kuishi madaktari hao kwani nyumba pamoja na idadi ya madaktari ni chache.
"Upungufu wa wataalamu na vifaa vya kutumia hospitali limekuwa tatizo kwetu"amesema Dkt.Breath
Ndug.Sabaya ameeka wazi kwamba fensi kujegwa pamoja na nyumba za madaktari ametoa ahadi iyo baada ya kuridhishwa na Majibu ya mganga mkuu wa wilaya ndug.Edward Lengai.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli