Kusimamia na kutekeleza hali ya upatikanaji wa maji katika majengo mbalimbali ya Taasisi zilizo chini ya Halmashauri ya Wilaya Monduli, mfano Ofisi kuu, Shule za msingi na za Sekondari za Serikali, Zahanati e.t.c
Kuwezesha na kufanya matengenezo madogo madogo ya miundo mbinu ya maji tatizo linapotokea katika maeneo mbalimbali ya sehemu nilizozitaja hapo juu ndani ya siku moja.
Kutoa Elimu katika jamii zilizokwisha jengewa miradi ya uvunaji wa maji ya mvua na uchimbaji wa visima ili viweze kuboreshwa na kutengenezwa kuwa katika hali bora ya usafi kwa matumizi ya afya ya binadamu.
Kusimamia na kutekeleza shughuli zote za maendeleo ya sekta ya maji kutoka Serikalini na kwa wadau wengine na kuzitolea taarifa kila robo ya mwaka na kuzituma Mkoani kwa wakati.