Wananchi katika Tarafa ya Kisongo Wilayani Mondul leo Agost 15, 2025 katika viwanja vya Ofisi ya Mtendaji Kata ya Meserani, wamempokea na kumkaribisha Mhe. Gloriana Mkuu wa Wilaya hiyo ili Kusikiliza na kutatua kero zinazo wakabili wananchi katika Tarafa hiyo.
Mhe. Gloriana ameelezwa kero mbalimbali zikiwemo. Kero za Wizi wa Mifugo na pikipiki, upungufu wa walimu mashuleni, uhaba wa Maji kipindi cha kiangazi, na changamoto za barabara.
Ambapo kero ya uhaba wa walimu, Wizi wa pikipiki na Mifugo, changamoto za barabara (TARURA) pamoja na changamoto ya uhaba wa Maji katika vijiji vya Tarafa hiyo zimetolewa utatuzi
Akiwasilisha kero ya maji Ndg. Pusindawa Mwenyekiti wa Kijiji cha Meserani ameomba kuongezewa mabwawa ya maji kwa ajili ya kunyweshea Mifugo kwani Moja lililopo huelemewa wakati wa kiangazi na kukauka huku akiomba miundombinu ya barabara kuelekea eneo la dampo ishughulikiwe kwa haraka.
Kuhusu suala la usafi wa Mazingira Meserani juu, Ndg. Fredrick Mnahela Afisa Mazingira Monduli ameeleza kuwa tiyari mzabuni amepatikana na ataanza kazi mara Moja kuanzia Agost 18, 2025.
Naye Bi. Lidya Mauki, (wa kwanza kulia) Afisa wa TAKUKURU Wilaya ya Monduli amewatahadharisha wananchi wa Tarafa hiyo juu ya suala la kupokea na kutoa Rushwa hasa kipindi hiki cha uchaguzi, ili waweze kumchagua viongozi wanaofaa na watakapsimamia haki zao.
Mhe. Gloriana amewasisitiza Wenyeviti katika Tarafa hiyo kukaa vikao vya kila mwezi vya Kijiji na kuwasomea wananchi mapato na matumizi huku akiwataka viongozi wa Chama kuwa na mahusiano mazuri na Watumishi wa Serikali kwa kuwa wote wapo ili kuwatumikia wananchi.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli