Idara ya Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii na Vijana ni kati ya idara za Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Idara ina vitengo vya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana, ambapo majukumu yake ni kuratibu na kusimamia upatikanaji wa huduma za jamii na utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika ngazi ya jamii. Katika utekelezaji wake Idara inaratibu mipango ya maendeleo ikiwa ni pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF - Tanzania Social Action Fund), Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa(CHF – Re-organized Community Health Fund), Mpango wa Kudhibiti UKIMWI, Mpango wa kurasimisha rasilimali na Biashara za Wanyonge wa Tanzania (MKURABITA), Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF), Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF) na Kuratibu asasi zisizokuwa za ki serikali (NGOs & CBOs) na vikundi vya kiuchumi.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli