Unapofika katika wilaya ya Monduli utapokelewa kwa taswira nzuri ya milima ya Monduli ionekanayo ikizungukwa na misitu ya kupendeza ni moja ya kivutio kikubwa kwa wageni wanaopenda kupanda milima. Upandaji wa milima hufanyika kwa kufika ofisi za Maliasili zilizopo Monduli baada ya kulipia kiingilio ambacho ni bei nafuu kwa Mtanzania atalipia Tsh 1500 ikiwa ni kiingilio na atapewa askari ambaye ni muongoza wageni ataambatana nae katika safari ya kupanda mlima. Kwa wageni wanaopenda kulala ndani ya misitu wataongeza Tsh 1500 ada ya malazi ndani ya hifadhi ya msitu iliyopo kwenye milima. Wageni wanatakiwa kuja na mahema yao, chakula na mahitaji mengine kama vinywaji. Wabeba mizigo wanaweza kupatikana ndani ya wilaya na kufanya makubaliano kulingana na mizigo itakayobebwa kupelekwa mlimani. Pia matembezi ya kawaida yanaweza kufanyika kuelekea katika maporomoko ya maji yaliyopo ndani ya hifadhi ya Milima ya Monduli.
Utalii wa Picha (Photographic Tourism)
Utalii wa aina hii hufanyika katika mapori yanayopatikana ndani ya wilaya ya Monduli na kwa sasa tunajivunia kwa kuwepo na Hifadhi ya Jamii ijulikanayo kwa jina la Randilen WMA. Watalii wanapata fursa ya kujionea wanyamapori kama Twiga, pundamilia, tembo, nyati, swala tomi, swala granti, ngiri, simba, kongoni, kuro pamoja na ndege wa kuvutia kama mbuni, tai, firigogo, chiriku na mandhari ya kuvutia iliyopo katika hifadhi hii inaonekana ukiwa katika view point ya mlima sandilen pamoja na picnic site iliyopo ndani ya eneo la Randilen WMA. Sehemu za kulala zipo kwa wageni wanaotembelea mbuga hii kuna lodges kama Tarangire Tree Tops, Nimali campsite, Ecoscience lodge ambazo zipo ndani ya WMA watalii wanapata malazi kwa bei nafuu na kufurahia huduma zitolewazo katika hotel hizo.kwa maelezo zaidi bofya hapa .fursa za uwekezaji monduli.pdf