Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kupitia Divisheni ya Mipango na Uratibu, leo Septemba 30, 2025 katika Ukumbi mdogo wa halmashauri hiyo imeendesha na kuratibu Mafunzo ya Mipango na bajeti kwa maafisa bajeti wa Divisheni na vitengo ikiwa ni maandalizi ya kuwa na uelewa wa pamoja juu ya masuala ya upangaji na utekelezaji wa Bajeti.Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Happiness Raphael Laizer, Ndg. Abraham Msofe ambaye ni Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo amewataka Maafisa Bajeti hao kuwa wasikivu na makini kwa muda wote wa mafunzo ili waweze kupata uelewa utakaowasaidia kufanya vizuri mara shughuli hiyo ya Mipango na bajeti itakapoanza.
Kwa upande wake Ndg.Danford Majogo Afisa Utamaduni Halmashauri ya Wilaya ya Monduli amesema kuwa, amefurahishwa na mafunzo hayo aliyoyapata yeye kama ajira mpya ambaye hakuwa na uelewa wowote juu ya zoezi la kuandaa Mipango na Bajeti sasa anaweza kufanya hivyo kwa kushirikiana na Mkuu wake wa Kitengo kwa Maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli