UTANGULIZI
Kitengo cha ukaguzi wa ndani kimeanzishwa chini ya kifungu 45 (1) cha sheria ya fedha ya mamlaka ya Serikali za mitaa Na 13 ya mwaka 1982.
Kitengo hiki kinatekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na Kamati ya Ukaguzi.Kitengo cha ukaguzi kina majukumu mbalimbali kama yalivyoainishwa hapa chini.
MAJUKUMU YA KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI
•Kukagua na kutoa ushauri sahihi ili kuboresha utawala bora
•Kufanya ufuatiliaji na ukaguzi na usimamizi wa fedha zote za Halmashauri zinakusanywa na halmashauri kwa kutumia mifumo ya kieletroniki.
•Kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha zote za Halmashauri na kuandaa taarifa kwa Afisa Masuuli.
•Kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na mali za Halmashauri pamoja na kuhakiki uwepo wa thamani ya fedha.
•Kuhakikisha malengo ya halmashari yanafikiwa na kuwa na uwajibikaji.
•Kuhakikisha kuwa sheria, kanuni na taratibu za fedha za serikali zinafuatwa kama zilivyo ainishwa kwenye sheria mbalimbali za serikali.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli