Halmashauri ya Wilaya ya Monduli imeibuka mshindi wa jumla katika mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa kwa mwaka 2025 baada ya kujinyakulia makombe 10 kutoka katika michezo mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bi. Happiness R. Laizer, ameipongeza timu ya Monduli kwa ushindi huo mkubwa, akiwashukuru Maafisa Elimu Sekondari, Afisa Michezo na walimu wote kwa mshikamano, juhudi na moyo wa kujituma uliozaa mafanikio hayo.
Bi. Laizer amepokea makombe hayo 10 kwa bashasha na furaha huku akisisitiza kuwa ushindi huo ni kielelezo cha uwekezaji madhubuti katika sekta ya michezo na elimu wilayani Monduli.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli