Utangulizi
Hali ya Kimuundo Idara ya ujenzi katika halmashauri ya wilaya ya Monduli
Idara ya Ujenzi inaundwa na vitengo vikuu vitatu kama ifuatavyo:
MTANDAO WA BARABARA
Wilaya ya Monduli inao mtandao wa barabara wenye urefu wa km 688 zinazohudumiwa na fedha za Mfuko wa barabara na vyanzo vingine. Aidha jumla ya Mtandao wa barabara wenye km 688 za barabara Wilayani Monduli kati ya hizo km 8.1 ni za Lami, km 138 ni za Changarawe na km 541.9 ni za udongo. Kwa ujumla km 186.01 (27%) ziko katika hali nzuri, km 245 (36%) ziko katika hali ya wastani na km 256.9 (37%) ziko katika hali mbaya.
UTEKELEZAJI WA MIRADI
Utekelezaji wa miradi ya Barabara kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara – (Road Fund)
Idara imeendelea kukamilisha kutekeleza kazi za miradi ya barabara iliyokuwa inaendelea ya mwaka 2015/2016. Aidha miradi ya mwaka 2016/2017 utekelezaji wake mikataba imeshasainiwa na kazi zinaendelea. Angali Jedwali A & B la utekelezaji
Utekelezaji wa miradi ya Majengo.
Idara inaendelea na usimamizi wa miradi yote ya Ujenzi wa miundo mbinu ya utawala, afya na Elimu yanayoendelea kujengwa.
Utekelezaji wa Kitengo cha Magari/Mitambo na umeme
Idara inaendelea kusimamia magari/mitambo na umeme ili kuimarisha kitengo kwa kubuni na kusimamia mitambo hii kidogo tuliyonayo. Aidha changamoto iliyopo ni Wataalamu wa Kitengo hicho kwasasa hawapo hasa upande wa Magari na Mitambo ila kwa upande wa Umeme tunaye Wataalamu wawili (Fundi sanifu umeme 2).
Bado tunaendelea kushauri mamlaka ya ajira na kuomba ajira ili kitengo hiki kiboreshwe kwa kuajiri Mhandisi wa Mitambo, mafundi sanifu na mafundi stadi wa magari/mitambo ili kuweza kuwa na uwezo hata wa kukagua magari kabla hayajapelekwa kwenye matengenezo na itapelekea kupunguza gharama ndani ya Halmashauri kwa kutengeneza Matengenezo madogo pia.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli