Hayo yamesemwa leo Septemba 10, 2025 na Mhe. CPA. Amos Gabriel Makalla Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli wakati akizungumza na Watumishi wakiwemo Maafisa Watendaji, Wenyeviti wa vijiji, Malaigwanani na viongozi mbalimbali wa Halmashauri hiyo.
Mhe. CPA. Amos Gabriel Makalla amempongeza Mhe. Gloriana Kimath Mkuu wa Wilaya ya Monduli kwa Kusikiliza na kutatua migogoro mbalimbali ikiwemo ya ardhi.
Akisoma taarifa ya Wilaya hiyo Mhe. Gloriana Kimath amesema kuwa, Wilaya hiyo imesikiliza jumla ya kero 50 za ardhi ambapo kero 11 zimesikilizwa na kutatuliwa na kero 39 zinaendelea kutafutiwa utatuzi ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa Elimu kwa Wananchi ili wawe na uelewa wa kutosha wa Sheria za ardhi, tafsiri ya mipaka na mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Mhe. Gloriana J. Kimath amuahidi Mhe. Makalla kuwa, yeye pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi, Malaigwanani (wazee wa kimila), viongozi mbalimbali na Watumishi wote watampa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha Wilaya ya Monduli na Wananchi wote wanakuwa salama na miradi ya maendeleo inakamirishwa kwa wakati.
Mhe. CPA. Amos Makalla amewasisitiza Watendaji na Kamati ya ulinzi na Usalama kuhakikisha kuwa kunakuwepo na amani na utulivu kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwakani Oktoba 29,2025 huku akisisitiza viongozi wa dini na Mila Kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha Wananchi kushiriki uchaguzi Kwa amani na utulivu.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli