Nina Imani mmejifunza mambo mengi tena ya msingi katika mafunzo haya mliyoyapata, Imani yangu kubwa kwenu ni kwamba mtahakikisha mnalinda amani na utulivu katika Jamii huku mkikiishi kiapo chenu.
Hayo yamesemwa leo Agost 27, 2025 katika Kata ya Engaruka na Mhe. Gloriana J. Kimath, Mkuu wa Wilaya ya Monduli katika hafla ya kufunga mafunzo ya Jeshi la akiba kundi la 43/2025; yaliyoanza rasmi April 1, 2025 na yanahitimishwa leo Agost 27, 2025.
Akisoma taarifa ya mafunzo hayo Meja Emmanuel John Shayo ambaye ni mshauri wa Jeshi la akiba Monduli amesema kuwa jumla ya vijana 64 wakiwemo vijana wa kike watatu (3) wanaohitimu hivi leo ni kati ya vijana 90 walioanza mafunzo hayo ambapo vijana 26 hawakufanikiwa kuhitimu kutokana na sababu mbalimbali.
Aidha, Meja Emmanuel John Shayo ameeleza kuwa lengo la mafunzo yaliyotolewa kwa vijana hao ni kwaajili ya kusaidia kuimarisha Ulinzi na shughuli mbalimbali za kiusalama ndani ya Jamii
Naye Ndg. Yohana Laizer mmoja wa wahitimu hao ameeleza changamoto mbalimbali walizokutana nazo wakati wa mafunzo ikiwemo changamoto ya kulipia vitambulisho, usafiri kuelekea maeneo ya mazoezi, chakula na kuchelewa kupata kombati.
Mhe. Gloriana Kimath amewapongeza wahitimu hao, wakufunzi wao kwa kuwaandaa vijana wa Kitanzania ili kusaidia kupambana na suala la Wizi, majanga ya moto na shughuli mbalimbali watakazoelekezwa kwa mujibu wa Sheria.
Mhe. Gloriana amehitimisha kwa kumwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kuweka Mazingira ya kuandaa mapema mavazi (kombati) kwa ajili ya vijana wa mafunzo hayo ili wawe wanamaliza mafunzo yao kwa wakati.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli