Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Happiness R. Laizer, leo Agosti Agost 15, 2025, amewaaga rasmi na kuwatakia kila la heri Watumishi wanamichezo wa Halmashauri hiyo wanaoelekea jijini Tanga kushiriki Mashindano ya Michezo ya Watumishi wa Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA) mwaka 2025.
Mashindano hayo, hufanyika kila mwaka yakihusisha Halmashauri 184 za Mikoa ya Tanzania yameanza rasmi Agosti 15 hadi 29, 2025.
Bi. Laizer amewapongeza wachezaji kwa kuchaguliwa kuiwakilisha Monduli na kuonesha matumaini makubwa ya ushindi kutokana na ongezeko la idadi ya wachezaji mwaka huu. “Mwaka jana tulishiriki kwa idadi ndogo, lakini mwaka huu tuna timu kubwa na naamini tutarudi na ushindi,” amesema Bi. Happiness Lazer.
Kwa upande wake, Ndg. Haruna H. Haji (wa pili kulia) Mkuu wa Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji ambaye ni kaimu Mwenyekiti wa Timu ya Wanamichezo, amemshukuru Mkurugenzi kwa kutoa vifaa vyenye thamani vya michezo na kuongeza idadi ya wachezaji huku akiahidi kuwa timu zote zitajituma ili Monduli irejee na ushindi mkubwa.
Bi. Happiness R. Laizer amehitimisha Kwa kumshukuru mdau kutoka Chama cha Walimu Monduli kwa mchango wa majitoleo ya maji kwa wanamichezo na kuwaombea afya njema, huku akiwahimiza kuwa na ujasiri na kujiamini ili kufanya vizuri katika mashindano hayo.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli