Hakikisheni mnasimamia upotevu wa vipindi pamoja na nidhamu kwa walimu na wanafunzi kwakuwa nidhamu nzuri ni chanzo cha ufaulu, na ikiwa mtazingatia ratiba ya vipindi na kuimarisha mikakati kuelekea mabadiliko makubwa ya ufaulu mliyojiwekea mtaboresha taaluma na ufaulu utapanda zaidi katika Wilaya ya Monduli.
Hayo yamesemwa leo Septemba 2, 2025 na Bi. Happiness R. Laizer Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli katika ukumbi mkubwa wa mikutano wa Halmashauri hiyo; wakati akizungumza na Maafisa Elimu Kata pamoja na Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari zilizopo Wilayani Monduli katika kikao kazi chenye dhima ya kuweka mikakati thabiti ya kuboresha na kuinua zaidi kiwango cha Taaluma katika Shule za Sekondari Wilayani humo.
Akisoma taarifa ya Elimu ngazi ya Sekondari Mwl.Given J. Moye ambaye ni kaimu Afisa Elimu Sekondari amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ina jumla ya shule 27 ambapo 16 ni za Serikali na 11 ni shule zisizo za Serikali.
Ambapo Mwl.Given ameeleza kuwa ufaulu katika Shule zote ni mzuri huku akibainisha matokeo ya mitihani ya Taifa kwa kidato cha pili na cha nne yanapanda mwaka hadi mwaka ambapo Mwaka 2023 ufaulu ulikuwa asilimia 97.8 na mwaka 2024 ufaulu umeongezeka na kufikia asilimia 98.85 na kupelekea kupata tuzo za pongezi kwa ufaulu mzuri wa viwango vya KPI kwa kidato cha pili nafasi ya kwanza (1) na kidato cha Nne nafasi ya tano (5) Kitaifa kati ya Halmashauri 184.
Kwa upande wake Kimbele Njake Mkuu wa Shule ya Sekondari Manyara, ameeleza mikakati inayotumika shuleni hapo kuhakikisha wanaondoa daraja "0" na daraja la "4" ikiwa ni pamoja kuhakikisha wanafunzi wanafanya mitihani kwa wingi ikiwemo mitihani ya marudio inayoshindanishwa ya kidato cha kwanza na pili kwa watahiniwa watarajiwa wa kidato cha pili pamoja mitihani ya marudio ya kidato cha pili na cha tatu kwa watainiwa wa kidato cha nne.
Naye Ndg.Raphael Martin Mkuu wa Shule ya Tumaini Senior Sekondari (binafsi) ameongeza kuwa mkakati wake ni kufanya mitihani kwa wingi hasa kutoka shule zinazofaulisha zaidi ikiwemo St.Francis ambapo hubadilishana uzoefu wa ufundishaji na ujifunzaji.
Sayuni Alex Tarimo Mwenyekiti TAHOSA amewaasa walimu wakuu wote kusikiliza kero na maoni ya wanafunzi kupitia vikao vya madarasa lakini pia kero za walimu wanazokutana nazo darasani na kusimamia mikakati wanaojiwekea ili kupata matokeo chanya.
Bi.Happness R. Laizer amehitimisha kwakuwataka walimu kufanya hamasa kubwa kwa walimu wenzao mashuleni ili wote kwa pamoja washiriki kikamiifu katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 202
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli