Mhe. Fredrick Edward Lowassa Mbunge wa Jimbo la Monduli June 26, 2025 amezindua mradi wa nyumba ya Wahudumu wa Afya ya mbili kwa Moja (two in one) yenye thamani ya shilingi milioni 92 katika Zahanati ya Kijiji cha Arkaria kilichopo katika Kata ya Sepeko Wilayani Monduli.
Aidha, Mheshimiwa Fredrick Lowassa amewapongeza wananchi kwa ujumla, Mkurugenzi, Watendaji wa Kijiji hicho pamoja na Mratibu wa TASAF kwa kushiriki na kusimamia vema ukamilishaji wa Mradi huo muhimu katika Kata hiyo huku Mhe. Fredrick akiahidi kuwapatia Maji ya Bomba kwa haraka ili kurahisisha huduma kwa wananchi na wagonjwa katika Kijiji hicho pamoja na ujenzi wa Barabara itakayo rahisisha usafiri.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo Bi. Cresensia Shine ambaye ni Mratibu wa TASAF Wilaya ya Monduli amesema " Mradi wa ujenzi wa nyumba ya Wahudumu wa Afya katika Zahanati ya Arkaria uliibuliwa na wananchi wa Kijiji hicho kwa Lengo la kuondoka changamoto ya makazi kwa Wauguzi wa zahanati ya hiyo na kuboresha huduma kwa wakati. Ambapo mradi huo umeanza Feb, 2025 na kukamilika mei, 2025. " amesema Bi. Cresensia
Naye Mhe. Diwani aliyemaliza muda wake Juni, 2025 ameishukuru kwa mambo mazuri ambayo TASAF imeyafanya katika Kata hiyo kwa kuwajengea zahanati na kwamba kaya masikini hazijaachwa nyuma kwa kuwa wananchi wengi wameendelea kunufaika na fedha zinazotoka katika mfuko wa TASAF.
Kwa upande wake Bi. Nasotwa Sangiki mnusaika wa Mfuko wa TASAF ameishukuru Serikari ya awamu ya sita inayoongozea na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaguza akina Mama wa Kata hiyo kwakuwa kupitia mradi huo vifo vya Mama na Mtoto vitaendelea kupungua kwani Wanawake wengi sasa wanajifungulia hospitalini.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli