Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Festo Shem Kiswaga(Ole Laizer) ameibuka mshindi katika mchezo wa mbio za mita 100 Kwa kushika nafasi ya tatu baada ya mshindi wa kwanza na wa pili, katika Bonanza la Michezo lililobeba dhima ya kuhamasisha Wananchi kujiandikisha na kupiga kura lililofanyika kata ya Mto wa Mbu viwanja vya Barafu leo Septemba 28, 2024 Wilayani Monduli.
Bonanza hilo limezinduliwa rasmi Leo na Mhe. Kiswaga na limehusisha wananchi wa rika tofauti katika Michezo ya mbio za mita 100, kukimbiza kuku, kukimbiza na magunia, kukimbiza na yai kwenye kijiko, kula mkate na soda dk. 2 na mchezo wapira wa miguu.
DC Kiswaga katika Bonanza hilo amehamasisha Wananchi wenye umri wa miaka 18 na kuendelea kujitokeza kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura huku akiwataka wote wenye umri wa miaka 21 na kuendelea wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi kujiandikisha na kuchukua fomu.
" Uchaguzi huu ni huru na wa haki, kila mwananchi anayo fursa ya kuchagua na kuchaguliwa hivyo hakikisha unajiandikisha ili uchague Kiongozi ambaye ni chaguo lako, na atakaye kufaa kukuongoza kwa miaka mitano(5). " Ameongeza kusema kuwa katika uchaguzi huu ws Serikali za Mitaa tunamchagua Mwenyekiti wa Mtaa, kitongoji na Mjumbe wa Halmashauri ya kijiji hivyo tujitokeze Kwa wingi tuchague viongozi wanaotifaa.
Aidha, DC Kiswaga ametoa angalizo kuwa Mwananchi yeyote atakaye fanya vurugu katika kipindi hiki cha uchaguzi kwamba atashugulikiwa kwakuwa nchi yetu ni ya amani na hivyo vurugu hazitakubalika.
Naye Bi. Jenipher Mapembe Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ametoa Rai kwa Wananchi wote Wilayani Monduli kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura lakini pia wenye nia ya kugombea wawahi kuchukuwa fomu mara tu zitakapotolewa Ili Kila mmoja ashiriki uchaguzi ifikapo Novemba 27, 2024.
DC Kiswaga amehitimisha kwa kwa kutoa shukrani kwa Maandalizi ya Bonanza hilo na amewataka viongozi walioandaa bonanza wafanye mazoezi hayo yawe ya mara kwa mara kwani yanachangamsha mwili ma kujenga Afya zetu.
Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli