Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Happiness Septemba 25, 2024 amefungua mafunzo ya siku tatu ya mradi wa Ustahimilivu wa Ardhi Afrika Mashariki: Masuluhisho ya asili(REAL NbS) wenye lengo la kuisaidia Jamii kupambana na uharibifu wa ardhi.
Akizungumza katika warsha hiyo Bi. Happiness R. Laizer ameeleza " Ni vyema na muhimu kuyatunza mazingira yetu yanayotuzunguka kwa kupanda miti ya kutosha na kuepuka suala la kutupa taka ovyo ili kuyalinda na kuyaweka mazingira katika hali ya usafi.
Naye Kiongozi wa mradi huo Tanzania Prof. Kelvin Mtei kutoka Chuo Kikuu Cha Nelson Mandela akiwa ameambatana na Prof. Jane Rickson kutoka uingereza amefafanua lengo la warsha hiyo kuwa ni kuwaleta Wadau wote pamoja ili kufahamiana, kujifunza na kwa pamoja kuchagua suluhisho zinaotokana na asili ambazo zitajaribiwa na kutumika wakati wa mradi, huku akiongeza kwamba tukishirikiana tutaweza kuzitekeleza suluhisho hizi.
Bi. Happiness R. Laizer amehitimisha kwa kuwataka Watumishi na Wadau mbalimbali kushilikiana vema na wataalamu wa mradi huo ili yale yote waliyojifunza katika warsha hiyo yaweze kuleta mabadiliko chanya katika kukabiliana na kuleta suluhisho la uharibifu wa ardhi.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli