Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Monduli Bi. Happiness R. Laizer aliyeteuliwa kusimama uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mujibu wa kanuni; amefungua mafunzo ya Uchaguzi kwa waratibu wa uchaguzi ngazi ya Halmashauri na Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya kata na vijiji kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024 Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli leo Septemba 30, 2024.
Akifungua mafunzo hayo Bi. Happiness R. Laizer amewataka wajumbe wote wa mafunzo hayo kuwa wasikivu na makini ili yale yanayofundishwa yakawasaidie kufanya kazi hii kwa usahihi zaidi na mafanikio mazuri. Ameongeza kusema " suala hili muhimu la uchaguzi liko mikononi mwetu kwani tumeaminiwa na Serikali na hivyo yatupasa kutenda kazi hii kwa umakini mkubwa. " amesema Bi. Happiness Laizer
Bi. Happiness amehitimisha kwa kutoa rai Kwa wajumbe wote wa mafunzo hayo kuwa wawe makini ili kazi hii iende vizuri na kuwataka wakawe mabarozi wazuri katika kutenda kazi hii muhimu.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli