Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi.Happiness R. Laizer ametoa maelekezo kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Wananchi wa Wilaya ya Monduli Leo Septemba 26, 2024.
Akitoa maelekezo hayo Bi.Happiness R. Laizer ametaja tarehe ya Uchaguzi, muda na mahali pa kujiandikisha ,Vituo vya kujiandikisha, Muda wakufungua na kufunga vituo hivyo, Muda na mahali pa kufanyia uchaguzi, sifa za mpiga kura pamoja na sifa za mgonbea, Uteuzi wa viongozi na ukataji wa Rufaa, Siku na utaratibu wa kampeni kuelekea Uchaguzi.
Kwa upande wa viongozi wa dini, Ndg. Ahmed Said amezungumza juu ya utayari wa viongozi wa Dini wa madhehebu yote kutoa elimu juu ya uchaguzi ili Kila mshirika wao mwenye sifa ajiandikishe na kupiga kura.
Sambamba na hayo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Ndg. Isaack Copriano amemshukuru Mhe.Dkt. Samia S. Hassan kwa kusisitiza uhuru kwa kila Chama kushiriki uchaguzi huu na kutoa ratiba kwa wakati ili watu watumie nafasi hii kijieleza.
Vile vile, Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Kiswaga ametoa marufuku Kwa vikundi vinavyoanza kuvuruga Wananchi na kuvuruga amani na kwamba Serikali haitakubaliana na jambo hilo.
Bi. Happiness R. Laizer amehitimisha kwa kutoa wito kwa Wananchi wote wa Wilaya ya Monduli wenye umri wa miaka 18 na zaidi, na wale wenye umri wa miaka 21 na kuendelea wajitokeze kushiriki na kuchukuwa fomu za kugombea bila kuathiri kanuni nyingine za uchaguzi.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli