Mbunge wa Jimbo la Monduli mhe.Fredick Lowassa ameendelea na ziara yake Wilayani Monduli kwaajili ya kukagua miradi ya maendeleo sambamba na kuzungumza na wananchi wa Monduli.
Akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Irikisongo Mhe.Fredrick Lowassa amewapongeza kamati ya ujenzi kwa jitihada walizozifanya mpaka kufikia hatua nzuri ya ujenzi wa bwalo la wanafunzi na kutoa shilingi milioni 2 kuunga mkono jitihada hizo zinazoendelea kufanyika.
Dorcas Lepunyu ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Irikisongo amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Monduli Kwa kutoa mchango ambao utaongeza kasi ya ujenzi wa bwalo hilo ili kuweza kutumika hivi punde.
Mbunge Fredrick, katika ziara yake amepata wasaa mzuri wakuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Monduli mjini soko la alhamisi baada ya kukagua mradi wa Barabara ya Sarakaoa na hospitali zilizojegwa kwa kiwango cha lami mita 430 zilizogharimu shilingi milioni 475 pamoja na kukagua mradi wa bwalo la shule ya Sekondari Irikisongo.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli