Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Festo Shem Kiswaga Desemba 20,2024 amezindua zahanati ya Oldonyo pamoja na nyumba ya watumishi 2 in 1 iliyopo Kata ya Lemoot.
Mhe.Festo Shem Kiswaga amewapongeza wananchi wa Kijiji cha Oldonyo Kwa nguvu kazi waliyotoa katika jitihada za ujenzi wa zahanati hiyo Kuanzia Msingi mpaka kukamilika kwa ujenzi huo.
Ameongeza kusema kuwa kwakuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt.Samia Suluhu Hassan imeleta fedha za ujenzi wa zahanati kwa kila Kata Wilayani Monduli, ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha majengo haya yanatuzwa kwaajili ya matumizi ya sasa na kwa vizazi vijavyo.
Naye Bi Happiness R. Laizer amewashukuru wananchi kwa majitoleo yao katika kuhakikisha ujenzi unaofanyika na kukamilika kwa wakati huku akiwaeleza na kutaja wingi wa fedha zilizotolewa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Wilaya ya Monduli na kwamba limebaki jukumu letu wananchi kurudisha fadhira mwakani Oktoba, 2025.
Kwa upande wake Ndg. Vicky Mollel mkazi wa kijiji cha Oldonyo amemshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa na watendaji wake wote katika Wilaya ya Monduli kwa kuwakumbuka akina Mama wa Oldonyo huku akiahidi kutoa hamasa kwa Wanawake wenzake kuanza kuhudhuria kliniki na kujifungulia katika zahanati hiyo na kwamba jambo hilo litapumguza vifo vya kina Mama wanaojifungilia nyumbani.
Mhe. Kiswaga amehitimisha kwa kusisitiza kwamba kwakuwa ujenzi wa zahanati ya Oldonyo umekamilika wakina mama wajawazito wasijifungulie nyumbani tena kwa kuogopa kutembea umbali mrefu kutafuta huduma badala yake waanze kupata katika zahanati hiyo huduma za kliniki hadi kujifungua, huku akiwasisitiza wahudumu wa Afya kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa na wazazi.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli