Afisa Uandikishaji Jimbo la Monduli Ndg. Emmanuel Richard Mpongo leo Desemba 8, 2024 katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii ( CDTI ) amefungua mafunzo ya siku mbili kwa Wasimamizi wasaidizi wa Vituo vya kujiandikisha na kuboresha taarifa katika daftari la kudumu la wapiga kura pamoja na wasimamizi wa bayometriki wa Vituo hivyo watakaofanya kazi hiyo katika Kata zote ishirini (20) zilizomo Wilayani humo.
Akizungumza na Wasimamizi hao Ndg. Mpongo amesema " Matokeo bora ya zoezi hili yanategemea zaidi umakini na uelewa wenu katika mafunzo haya mtakayopatiwa leo; hivyo ninawasihi muwe na ushirikiano nzuri na wa karibu na Tume iliyopo hapa Monduli kwa wakati wote wa zoezi hili na kwa ufafanuzi au maelekezo yoyote , msisite kutoa taarifa muwapo vituoni ili mpatiwe msaada kwa haraka kwa ufanisi ulio bora."
Aidha, Ndg. Mpongo amewaasa Wasimamizi wasaidizi wa Vituo vya uandikishaji hao kwamba kwa kuwa waapa viapo vya Uaminifu na Uadilifu wazingatie zaidi maelekezo na kufanya kazi kwa weledi huku akisisitiza utunzaji wa vifaa vyote vya uandikishaji kwa kuwa bado vinahitajika kutumika katika maeneo mengine nchini.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli