WATOTO AMBAO HAWAJAANDIKISHWA KWA WAKATI,WAKAMATWA MACHUNGANI NA KULETWA HALMASHAURI YA WILAYA YA MONDULI.WAPELEKWA SHULENI.
Watoto hao ambao Idadi yao ni kumi na nane (18) ikiwemo wavulana tisa (9) na wasichana (9) walikosa kuandikishwa kwa umri uliostahili machungani na kuletwa Halmashauri ya wilaya ya Monduli na kupelekwa shule ya Msingi ya bweni Engaruka juu yenye kituo cha kufundishia cha MEMKWA.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Ndug. Adili Mwanga ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Maliasili na uhifadhi wa mazingira amepokea michango ya fedha kutoka kwa watumishi mbalimbali mapema leo mchana na kumkabidhi Mkuu wa divesheni Elimu Msingi Bi.Natang'aduak Mollel ili kukidhi mahitaji kwa wanafunzi sita (6) ambao hawakupata mahitaji.
Mkuu wa divisheni Elimu Misingi, amemshukuru Mkurugenzi mtendaji Bi.Happiness R. Laizer pamoja na watumishi wa halmashauri,CMT,Waratibu Elimu Kata,Walimu Wakuu kwa majitolea yao ya mahitaji ya watoto ya shule ikiwemo tranka,sare za shule,madaftari,mafuta na sabuni.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha mawasiliano serekalini
Monduli
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli