Mkuu wa wilaya ya Monduli, Mhe. Idd Hassan Kimanta amekabidhi jumla ya pikipiki 20 kwa waratibu elimu kata 20 wa kata zote za wilaya ya Monduli. Tukio hili lilifanyika leo tarehe 11/10/2018 katika sherehe ya kukabidhi vyombo hivi vya usafiri kwa waratibu elimu kata katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Monduli.
Awali ,Mkurugenzi Mtendaji (w) Ndugu; Stephen A. Ulaya alikabidhiwa Jumla ya pikipiki 20 na Mkuu wa wilaya ili awakabidhi waratibu elimu kata 20 wa kata zote za Monduli kwa utaratibu maalumu.
Wakati akisoma taarifa Afisa Elimu msingi Bi. Theresia kyara alisema kuwa pikipiki hizi zimenunuliwa na serikali kupitia program ya LANES (Literacy and Numeracy Education Support) kitaifa. LANES ni mpango wa kukuza stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.
Mh. Kimanta ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika sherehe hizi za makabidhiano alisisitiza katika matumizi mazuri na sahihi ya pikipiki hizi kwa wahusika. Alisema pikipiki hizi zitakuwa msaada mkubwa katika kuhakikisha kuwa; waratibu wanafanya ukaguzi wa ndani wa ufundishaji kwa ustadi kwa waalimu wao na kufanya ziara za kushtukiza mashuleni ili wajionee hali halisi ya ufundishaji.
Pia pikipiki hizi zitasaidia kuthibiti utoro kwa wanafunzi kwa kutembelea serikali za vijiji ili kutoa miongozo kwa wazazi/walezi wanosababisha utoro kwa wanafunzi pamoja na kutembelea shule mara kwa mara ili kusikiliza na kutatua changamoto za waalimu na wanafunzi.
Wilaya ya Monduli ina shule za msingi za serikali 60 na jumla ya wanafunzi katika shule hizi ni 32,954 wakiwemo wavulana 16,683 na wasichana 16,201.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli