Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe Festo kiswaga Leo Oktoba 11, 2024 amefanya uzinduzi rasmi wa zoezi la uandikishaji wa daftari la orodha ya wakazi katika kituo cha Monduli mjini (Magharibi) Kilichopo eneo la soko la kila siku la Monduli mjini.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Festo Shem Kiswaga ametaja jumla ya vituo 238 kuwa vimetegwa kwa ajili ya watu kwenda kujiandikisha ambapo katika zoezi hili tunatarajia jumla ya watu 132,923 watajiandikisha katika daftari la orodha ya wakazi wa Monduli.
Aidha Mhe.Kiswaga amewataka Wananchi kujitokesa kwa wingi kujiandikisha.
"usipojiandisha katika daftari la orodha ya wakazi maana yake ni kwamba hutaweza kupiga kura. Na zoezi hili linaloanza leo linaanza rasmi na mimi kwani nitajiandikisha hapa hapa kwakuwa ndicho kituo changu cha kujiandikisha". amesema DC kiswaga.
Naye Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Monduli ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo Bi. Happiness R. Lazier ametoa wito kwa Wananchi na watumishi wa umma kwenda kujiandikisha katika vituo vilivyopo katika maeneo yao ya makazi huku akieleza kuwa hiyo ndiyo fursa pekee itakayo wawezesha kupiga kura siku ya Novemba,27 2024.
Aidha Bi Happiness Laizer amewataka Wananchi kutochanganya suala la daftari la orodha ya wakazi na daftari la kudumu la wapiga kura na kusema tutumie fursa ya kwenda kuhakiki jina kabla ya siku ya Uchaguzi ili tusiikose fursa ya kupiga kura Novemba 27,2024.
Vilevile Ndg.Isack Joseph Copriano Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli amewaeleza wananchi kuwa vitambulisho walivyo navyo havitatumika kupiga kura hivyo wajiandikishe na pia amesema watu wasio wa maeneo hayo wasijiandikishe bali wafanye hivyo katika maeneo wanayoishi ili wapate kuchagua viongozi watakaofaa kuleta maendeleo katika maeneo yao na Tanzania kwa ujumla.
Kwa upande wake Bi. Regina Martin Mkazi wa Monduli mjini amewataka wanawake kujitokeza kujiandikisha kwa wingi sambamba nakuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwani wanawake wanaweza.
Akihitimisha DC Kiswaga amesema mtu yeyote atakae jaribu au kufanya utani kwenye suala la kujiandikisha Mkono wa Sheria utamfuata.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli