Serikali ya Awamu ya sita imetoa kiasi cha shilingi Billion 2.8 kwa kipindi cha Mwaka wa fedha 2024/25 kwaajili ya kutekeleza Miradi 11 ya Maji Katika vijiji 13 vya wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kwa lengo la kumaliza tatizo la Maji kwenye vijiji vyote 62 Ambapo vijiji 45 vimekishwa Pata Maji Safi na Salama na kufikia asilimia 69 ya upatikanaji wa Maji Safi na Salama kwa wilaya hiyo.
Akifungua Mkutano Mkuu wa Pili wa vyombo vya Utoaji huduma ya Maji ngazi ya Jamii (CBWSOs), Mkuu wa wilaya ya Monduli festo Kiswaga ameleza kukamilika kwa Mradi hiyo itafikia Asilimia 86 ya upatikanaji wa Maji Monduli na kupunguza tatizo Hilo la Maji.
DC Kiswaga ameeleza dhamira ya serikali ni kuwapatia Huduma ya Maji kwa wananchi, hivyo ni wajibukulinda Miundombinu ya Maji pamoja na ulipaji Ankara za Maji.
Awali,Mhandisi Neville Msaki Meneja wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira vijijini RUWASA ameleza Hali ya mwendeno wa uendeshaji wa skimu za Maji.
Kwa upande mwingine baadhi ya Vyombo vya watumia Maji na viongozi huleta changamoto ambapo jumla ya vyombo vya watoa huduma ngazi ya jamii 20 vilivyoudwa na kusajiliwa kwa sheria na.5 ya mwaka 2019.vyombo 10 vimeendelea kutekeleza majukumu kama inavyotakiwa ambavyo ni mto wa mbu,Lolkisale,Makuyuni,Naitolia,Mswakini juu,Naiti,Meserani bwawani,Selela,Mbaashi na Saruni Oldonyo.Vyombo sita vinafanya kazi kwa kusuasua ambavyo ni Monalo,Mfereji,Enguik,Lendikinya,Emairete,Eluwai,na Lemoot.ambapo vyombo viwili avijanza kufanya kazi kabisa ni Mswakini chini,na Engaruka.na vyombo vipya ni viwili.Lepuruko na Nafco.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli