Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan , amempigia simu mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda na kutaka kujua hali inayoendelea katika uzinduzi wa kambi ya madaktari bingwa na wabobezi mkoani humo.
Akizungumza kupitia simu, Rais Samia amemuhakikishia RC Makonda kuwa ataongeza nguvu kubwa katika kambi hiyo kwa maslahi mapana ya kuendelea kutolewa kwa huduma bora kwa wananchi wa Arusha.
Vilevile, Rais Samia ametoa wito kwa wananchi wa Arusha kutumia fursa hiyo vizuri katika kujitokeza kwa wingi kwenye ushiriki wa kupata huduma hizo za afya.
Aidha, Rais Samia ametoa pongezi kubwa kwa Hospitali zote, Taasisi za Afya na Mashirika yote ambayo kwa pamoja wamekubali kushirikiana na RC Makonda katika kutoa huduma bure kwa wananchi kwa siku zote 7 (Juni 24 - 30, 2024)
Naye RC Makonda amemsisitizia Rais Samia kuwa wananchi wa Arusha wana imani kubwa na serikali yake anayoiongoza na kuendelea kumuunga mkono wakati wote.
Pia , RC Makonda amembainishia Rais Samia kuwa katika kambi hiyo ya madaktari bingwa na wabobezi, wapo madaktari na wauguzi 450, Helikopta moja ya kubebea wagonjwa mahututi kwaajili ya kuharakisha kuwafikisha katika huduma za kimatibabu zaidi pamoja na Ambulance 8.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli