Mhe.Naibu Waziri wa maji
Injinia Kondo Andrea mathew Ameyasema hayo kwenye ziara yake ya kutembelea miradi ya maji Wilayani Monduli katika kijiji cha Emairete,kitongoji cha Emorijo Leo tarehe 15.6.2024.
Ambapo Naibu waziri wa maji,amemsimamisha mkandarasi wa kampuni ya LUKOLE kuendelea na kazi ya ujenzi wa bwawa la Soimineni lililoko katika kijiji cha Emairete kitongoji cha Emorijo kwa kuwa na hali ya uzembe kazini na kutofanya kazi ndani mkataba aliopewa,ambapo mkataba ulianza kufanya kazi tangu mwenzi juni 2023 mpaka kufikia Leo tarehe 15.6.2024 kazi hiyo kufikia asilimia 12% pamoja nakuongezewa muda wakufanya kazi hiyo na kupewa fedha kiasi cha shilingi milioni 23.7 kama kianzio cha kufanya kazi hiyo.
Hali ambayo imeonyeshwa kutokuridhika na utendaji wa kazi wa mkandarasi huyo baada ya mhe.Naibu waziri kumuuliza maswali ya papo kwa hapo nakushidwa kutoa majibu kamili kwakuonyesha hali ya kusuasua katika majibu yake.
"Nimarufuku mkandarasi ambaye ameaniwa nakupewa dhamana kubwa yakufanya kazi kuchezea pesa za serikali kwa namna yeyote ile "amesema Naibu waziri mhe.Kondo.
Bwawa hilo la Soimineni lililopo kijiji cha Emairete linalo gharimu Gharama ya shilingi bilioni 1.6 ambapo vijiji jirani vitaenda kunufaika na mradi huo na kuondokana na adha ya shida ya kufwata maji kwa umbali mrefu.
Naibu waziri wa maji ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa jitahada zinazofanyika kwakuleta miradi mikubwa ya maji wilayani Monduli.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli