Baraza la Madiwani Wilayani Monduli limetoa pongezi Kwa kamati ya Elimu Afya na maji pamoja na waataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Kwa usimamizi mzuri wa ukarabati wa shule kongwe za Msingi ikiwemo Shule ya Msingi Monduli juu, Shule ya Msingi Mazoezi na Shule ya Msingi Mto wa Mbu.
Pongezi hizo zimetolewa Mei 14, 2025 na Baraza hilo lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momduli mara baada ya wasilisho la kamati hiyo lililowasilishwa na Mwenyekiti wake Mhe. Loth Tarakwa; ambaye ni Diwani wa Kata ya Meserani Wilayani Monduli.
Aidha, Mhe. Loth kupitia wasilisho lake, amesema, kwakuwa Halmashauri ina shule kongwe nyingi Kuna uhitaji mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kuendelea kufanya ukarabati wa shule nyingine kongwe ili shule hizo ziwe na mazingira bora kwa walimu kufundisha lakini wanafunzi kujifunza.
Sambamba na hilo, Mhe. Loth ameshauri Baraza hilo kuendelea na suala la ukarabati wa maabara katika shule za Sekondari za Mswakini na Meserani ili kuboresha mazingira ya ujifunzaji kwa vitendo kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi kwa kuwa tunatarajia mwakani Kuwa na wanafunzi wa kidato cha tatu.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli