Wananchi na Jamii kwa ujumla wametakiwa kutunza miundo mbinu ya Shule inayokengwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan na kuwa Mstari wa mbele kihakikisha wanafunzi wanapata Elimu.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Divisheni ya Elimu Msingi Wilaya ya Monduli Bi Natang'aduaki Mollel akizungumza na wanachi wa Kata ya Loksale kitongoji cha Endarpoi baada ya kuzindua Rasmi shule mpya ya Msingi Endarpoi katika kata hiyo.
Amsema ni wajibu wa Wazazi kushirikiana kwa pamoja na waalimu kutunza miundombinu ya Shule hiyo kwa kujali usalama na usafi wa Majengo hayo ili kuishawishi serikali kuwaongezea huduma zingine za kimaendeleo.
Katika hatua nyingine amewataka Wazazi kuwa mstari wa mbele kuwapekeleka watoto shuleni bila kujali jinsia kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha jamii nzima inapata elimu bora kwa usawa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Elimu, Afya na Maji wilaya ya monduli ambae pia ni diwani wa kata ya Mesearan wilayani hapo Mhe. Lotti Naparana ametumia mkutano huo kukemea mila potofu za kuozesha mabinti wadogo badala ya kuwapekeleka Shule.
Akisoma Risala kwa mgeni Rasmi Mkuu wa shule hiyo Amesema miongoni mwa Changamoto zinazo wakabili katika shule hiyo ni Uhitaji wa Thamani kama Viti na meza katika ofisi za walimu pamoja na Uhaba wa waalimu wenyewe kutokana na shule hiyo kuwa na Wawili na wanafunzi zaidi ya mia mbili.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli