Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha imeadhimisha Siku ya magojwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Duniani Januari 30, 2025 katika Shule ya Msingi Ngarash, Kwa kutoa Elimu kwa Wanafunzi pamoja na Wananchi katika zahanati zilizopo Wilayani Monduli.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Bi.Jubilate Temu ambaye ni mratibu wa magojwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele Wilayani Monduli kwa niamba ya Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. George Kasibante amesema Maadhimisho hayo yemelenga kuikumbusha jamii kwa ujumla pamoja na Wanafunzi jinsi ya kujikinga na magojwa hayo yaliyokuwa ayapewi kipaumbele kama Minyoo, Trakoma, kichocho pamoja na mengine.
Kwa upande wake Bi.Joyce Shangai ambaye ni mjumbe wa kamati katika magonjwa yaliyokuwa ayapewi kipaumbele amewaeleza wanafunzi kuchukua tahadhari zote dhidi ya magojwa haya Kwa kuzingatia usafi wao wenyewe na kuacha kujisaidia hovyo kwenye mazingira yasiyo rafiki.
Naye Gladness Robert ambaye ni mwanafumzi wa shule ya Msingi Ngarash amewaasa wanafunzi wenzake kuchukua hatua za kujikinga na magojwa hayo Kwa kuhakikisha wanatumia dawa za minyoo na kuepuka kula bila kunawa mikono na kuacha kujisaidia hovyo.
Akihitimisha maadhimisho hayo Bi.Jubilate Temu amewasisitiza wanafunzi Kuwa wasafi na kuzingatia sana Kinga tiba ili kuweza kukwepa magojwa hayo ambayo yaliyokuwa ayapewi kipaumbele.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli