Mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti UKIMWI Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mhe.Richard P. Laizer (Diwani wa Kata ya Selela) Leo Feb 3, 2025 ameongoza kikao cha kamati hiyo katika ukumbi wa Halmashauri chenye lengo la kupokea na kujadili mapendekezo ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Akiwasilisha mapendekezo ya mpango wa bajeti ya Idara ya Afya,Ustawi wa jamii na Lishe Dr.Sanema Guulo ameeleza malengo matatu (3) ambayo Idara inatarajia kuyafikia kuwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanaoisha na VVU wanafahamu hali zao,wanaogundululika Kuwa kuwa na maambukizi kuanza dawa kikamilifu Kwa wakati pamoja na kupunguza virus kwenye damu kwa wanaotumia ARVs.
Aidha Dr.Sanema ameeleza kuwa ili kuyafikisha malengo hayo Idara imejipanga kushirikisha wadau mbalimbali Wilayani humo huku hamasa ikitolewa zaidi kwa Wananchi kupima na kufahamu hali ya afya zao.
Kwa upande wake Bi.Aimosaria Minja kaimu mkuu wa Kitengo Cha maendeleo ya jamii,Ustawi wa Jamii na vijana amebainisha lengo kuu la Idara hiyo Kuwa nikuhakikisha huduma ya UKIMWI inaboreshwa na maambukizi mapya yanapungua kwa Jamii.
Mhe.Richard Laizer amehitimisha kikao hicho kwa kuwashukuru wajumbe kwa michango yao na kuwataka kuendelea kusimamia malengo yaliyowekwa kwa kuendelea kupambana na changamoto za maambukizi mapya ya VVU.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli