Mhe. Isack Copriano Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ambaye pia ni Diwani wa Monduli Mjini, ameongoza Baraza la kawaida la madiwani la robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2024/2025 lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Ambapo, katika Baraza hilo Mhe. Isack Copriano ameruhusu maswali na majibu ya papo Kwa hapo ambayo yameibuliwa kutoka Sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Maji, pamoja na ukarabati wa miundombinu ya Barabara huku maswali mengine yakiulizwa na kujibiwa kuhusu miundombinu ya nishati ya umeme katika baadhi ya Kata Wilayani humo.
Akizungumzia suala la uhaba wa walimu katika Shule za Msingi Mhe.Paulina Richard Diwani viti maalumu Tarafa ya Kisongo ameshauri wataalamu kupeleka maombi ya uhitaji wa walimu ili kupata walimu wa kutosha kwa kuwa Shule nyingi Wilayani humo zimekuwa na idadi kubwa ya Wanafunzi, huku idadi ya walimu ikiwa ndogo suala linalopelekea utendaji kazi kuwa mgumu na hata Matokeo kutofikia Viwango vilivyopendekezwa.
Naye Mhe.Loth Diwani Kata ya Meserani ameongoza kwa kusema kuwa uhitaji wa walimu wa Sayansi pia ufikiriwe kuweza kuweka mazingira rafiki ya usomaji Kwa Wanafunzi na ufanisi mkubwa hasa katika masomo ya sayansi.
Kwa upande mwingine Ndg. Ramadhani Madeleka kutoka Mkoani, ameshauri suala la utaratibu mzuri wa uendeshaji wa maswali yanayoulizwa kwenye Baraza kuwa yawasilishwe mapema kwa wataaamu ili waweze kuyachakata nakutoa majibu yaliyosahihi kwa wakati.
Kwa upande wa Miradi, kuhakikisha tathmini inafanyika katika miradi yote inayotarajiwa kufanyika iIi kwenye bajeti zitengwe fedha ambazo ni gharama halisi itakayo kamilisha mradi husika kwakufanya hivyo itasaidia kutokuwa na Miradi kipolo.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli