Mhe.Festo Shem Kiswaga Mwenyekiti wa kamati ya Lishe Wilaya ya Monduli, leo Januari 31, 2025 ameongoza kikao cha kamati hiyo Kwa robo ya pili ya Oktoba - Desemba 2024/2025 chenye dhima ya kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe katika Kata zote Kwa robo hiyo.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe katika Idara ya afya Wilaya ya Monduli Bi.Adventina - Afisa Lishe zahanati ya Mto wa Mbu ameeleza shughuli mbalimbali zilizofanyika katika robo hiyo; ikiwemo kutoa elimu ya Lishe kwa makundi mbalimbali katika jamii, kushiriki maadhimisho ya siku ya Lishe duniani pamoja na kutoa tathmini ya hali ya lishe Wilayani humo.
Akizungumzia hali ya Lishe kwa watoto Bi. Adventina amesema jumla ya watoto 32,426 waliochunguzwa watoto 8 walikutwa na utapiamulo, huku watoto 14 hali zao za Lishe zikibainika kuwa hafifu na mtoto mmoja akithibitika kuwa na hali duni ya Lishe.
Kwa upande wa Suala la chanjo na vitamini Bi Adventina ameeleza kuwa jumla ya watoto 101 walipewa vitamin "A", 61 walipewa dawa za minyoo na 56 walipata chanjo ya PCV, PENTA na SURUA. Aidha, jumla ya watu wazima 67 Waliopima hali ya lishe wawili(2) walithibitika kuwa na uzito pungufu, 25 uzito uliozidi na wanne(4) uzito uliothibitika kupitiliza huku watano (5) wakithibitika kuwa na shinikizo la juu sana la damu.
Kwa upande wake Dkt. George Kasibante ambaye ni Mganga Mkuu wa Wilaya kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji amesema, mabadiliko chanya yaliyoleta matokeo mazuri yametokana na kuwawezesha watumishi walioko katika vituo vya afya kuwa na Mazingira mazuri ya Kazi, uwepo wa Dawa na Vifaa tiba katika Hospitali na zahanati zote ndani ya Wilaya ya Monduli, huku akizitaja changamoto chache zilizopo na kuahidi kuzitafutia majawabu.
Akihitimisha kikao hicho, Mhe. Kiswaga Mwenyekiti wa kamati ya Lishe ya Wilaya, amewaasa Watendaji wa Kata katika Wilaya ya Monduli kujibidiisha na kusimamia shughuli za lishe na afya Kwa ujumla ili kuimarisha afya za wananchi katika maeneo yao wanayofanyia kazi.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli