DED amewapongeza timu ya Halmashauri ya wilaya ya Monduli iliyoshiriki mashindano ya watumishi wa mamlaka za serikali za mitaaa (SHIMISEMITA),yaliyofanyika Jijini Mwanza ambapo Monduli imeibuka kuwa mshindi wa nafasi ya pili kwa uchoraji kitaifa.
Sambamba na hilo Mkurugenzi Mtendaji amepongeza pia jitihada zilizofanyika na timu hiyo mpaka kuingia nafasi ya 16 bora katika mchezo wa (handball) mpira wa mikono,na kuingia katika robo fainali katika mchezo wa karata,pamoja na kushika nafasi ya nne (4) katika mchezo wa kurusha tufe kitaifa.
Vivyohivyo Mkurugenzi amewapongeza wachezaji walioenda kushiriki katika mashindano ya (SHIMISEMITA) kwani ni Halmashauri zaidi ya miamoja (100) zimeshiriki mashindano,na hawajapata Makombe na sio tu kupata ushindi bali hata Halmashauri nyingine hazijashiriki kabisa,hivyo kwa Monduli mmepata nafasi ya kushiriki na kurudi na ushindi wa nafasi ya pili kwa uchoraji kitaifa.
Mashindano hayo yalianza kuanzia Oktoba 26, 202, yaliyobeba kaulimbiu ya "shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ujenzi wa taifa endelevu."
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli