Shirika lisilo la kiserikali la TUSONGE linalodhaminiwa na UN WOMEN linalofanya kazi zake Wilayani Monduli , Oktoba 30, 2024 katika eneo la Meserani Wilayani Monduli limeungana na mashirika mengine kimataifa kuadhimisha siku ya kuleana na kusaidiana kwa Wanawake na Wanaume kiuchumi, kisiasa na kiongozi ikiwa ndio dhima ya msingi ya ya Shirika hilo ili kuleta maendeleo chanya katika maisha ya Mwanamke na Mwanaume katika jamii.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Bi. Aimosaria Minja Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Monduli ametoa shukrani kwa Shirika la TUSONGE kwa kuendelea kuwawezesha Wanawake wa Meserani kwani imesaidia Wanawake wengi kutambua haki zao na fursa mbalimbali katika maisha na kuweza kujikwamua na kusonga mbele kwa kutunza, kusomesha na kulea familia zao huku akihimiza ushirikiano katika malezi kati ya Wanawake na wanaume sambamba na kujishughulisha na shughuli za ujasiliamali na kujipatia kipato.
Naye Elibrenda Mwakio ambaye ni Mratibu Msaidizi wa mradi huu Mkoa wa Arusha amesema " Sisi wanawake ni vyema tukaungana na wenzetu Kimataifa kuadhimisha siku hii ya kusaidiana na kuleana kwani ni siku muhimu ya kumheshimisha Mwanamke nami kama mwanamke imeniheshimisha, hivyo natoa wito kwa wanaume na watoto wa kiume kuweze Kuona akina mama ni nguzo ya kidunia na wanapaswa kupewa heshima inayostahili.
Kwa upande wake Bi. Eva Meleji mkazi Kata ya Meserani ameshukuru Kwa kunufaika na mambo mbalimbali waliyopata kupitia Shirika la TUSONGE kwa mada nzuri ambazo kimsingi zimewajenga katika suala Zima la kuleana na kusaidiana na wenza wao kwani itasaidia jamii kuishi kwa upendo na kuleta maendeleo.
Bi. Aimosaria Minja amehitimisha maadhimisho hayo kwa kuhimiza ushirikiano na mshikamano katika kuleana na kusaidiana ili amani na upendo vidumu katika familia na kuchochea maendeleo binafsi na Taifa kwa ujumla.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli