Akizungumza na walimu wa shule za msingi katika kikao hicho amewaasa walimu kuwa na uwezo mkubwa katika ufundishaji wao ili kuweza kupandisha kiwango cha ufaulu mzuri.
Aidha bi.Natang'aduak amewashukuru waalimu kwa kuweza kusimamia vizuri MEWAKA kwani kupitia mewaka wanafunzi wameongeza uwezo na kiwango cha ufaulu mzuri.na ndio maana mpaka sasa kupitia "mewaka day"imeekwa kwa sababu ya kufundisha wanafunzi kuwa na uwezo zaidi nje ya darasa.
Hata ivyo amewaaidi walimu kuwa 2.2.2024 kutakuwa na pongezi kwa shule ambazo zilizofanya vizuri bila ya kutumia viboko kuwachapa wanafunzi.watapewa zawadi pamoja na waalimu wa shule hizo kwa ujumla.na pia mpaka sasa shule ambazo zimeingia katika vin'yanganyiro ni mbili (2).
Amewashukuru waalimu wa shule za msingi kwa usimamizi mzuri wa miradi ambayo Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania @samia_suluhu_hassan ameleta fedha nyingi kwa ajili ya miradi hiyo ya maendeleo.hivyo basi wilaya ya monduli jukumu letu ni kuitunza miradi yote kwa weledi.
Imeandaliwa na kitengo cha mawasiliano serekalini
Monduli
#Kazi Iendelee
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli