Mhe. Mrisho Gambo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha amekemea vikali tabia ya watu waaotumia madaraka vibaya kujipatia ardhi kinyume na sheria. Akizungumza katika baraza la maalumu la madiwani kuhusu uvamizi wa msitu wa Lendikinya uliopo wilayani monduli, amesema “sheria ifuate mkondo wake, haijalishi mtu ni nani na ana historia gani. Kumezuka tabia ya watu wa Monduli kuwa wanapopata uongozi wanatumia nafasi zao kujipatia ardhi kinyemela”
Imegundulika kuwa kuna baadhi ya wananchi wamejipatia hati za umiliki wa mashamba ndani ya msitu wa serikali wa Lendikinya. Mhe gambo amemuagiza mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Idd Hassan Kimanta kuhakikisha waliovamia msitu wa lendikinya uliopo eneo la Monduli juu waondoke na kupisha eneo la msitu kwa manufaa mapana ya wananchi, Na wale wote wliohusika kutoa hati hizi kinyume na kanuni na taratibu wachukuliwe hatua kali.
Figure 1 Mkuu wa Mkoa wa Arusha akiongea katika baraza la madiwani
Pia, Gambo aliwapongeza viongozi wa Wilaya ya Monduli akiwemo Mkuu wa wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri (Isaack Joseph Copriano) na Mkurugenzi Mtendaji (w) (Ulaya, Stephen Anderson) kwa kupata hati safi ya ukaguzi kwa mwaka 2016/2017 na kufikia lengo katika ukusanyaji mapato ya ndani ya Halmashauri. Mapato yaliyokusanywa kwa mwaka 2017/2018 hadi kufikia June 19, 2018 yamefika asilimia 97 ya bajeti. Gambo amesisitiza kuwa mpaka kufikia mwisho wa mwezi june 2018 halmshauri inatakiwa iwe imefikia asilimia 100 ya ukusanyaji wa mapato yake ya ndani ya Halmashauri. Amesema Halmashauri itambue fursa zingine za mapato ili iweze kukusanya zaidi kusudi iweze kutoa huduma kwa wananchi vizuri. Pia, ameipongeza Halmashauri kukubali jitihada za serikali ya Rais John Joseph Magufuli kuhusu elimu bure na kuagiza viongozi wa wilaya kuhakikisha fedha za elimu bure zinatumika ipasavyo.
Mh. Mrisho Gambo katika ziara yake wilayani Monduli amehudhuria kikao cha baraza maalumu la madiwani linalohusu kujadili majibu ya halmashuri juu ya hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za zerikali. Shughuli nyingine alizozifanya ni pamoja na kufungua shule ya msingi Lengijape iliyopo kata ya Lemooti, kuusikiliza pamoja na kutatua kero mbalimbali za wananchi katika kata ya Lemooti na Lolksale.
Imeandikwa na
E.msifuni,
Afisa TEHAMA (W),
Monduli.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli