UN WOMEN kwa Kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Januari 8, 2025 katika Kata ya Naalarami wamefanya shughuli za utekelezaji Kwa Maendeleo ya Jamii katika kumuinua Mwanamke Kiuchumi, kisiasa na kiuongozi, ikiwa ndio dhima ya msingi ya Shirika hilo ili kuleta maendeleo chanya katika maisha ya Mwanamke katika jamii.
Akizungumza katika mdahalo wa viongozi wa mila (malaigwanani) pamoja na viongozi wa dini juu ya masuala ya kijinsia juu ya haki, uongozi, uchumi, kwa wanawake Bi. Aimosaria Minja ambaye ni mratibu wa UN WOMEN amewataka wanawake wa kata hiyo kuendelea kufanya shughuli za maendeleo mbalimbali zinazoweza kuwainua Kiuchumi ikiwemo kucheza vikoba ili kuweza kuwekeza fedha zitakazo waletea maendeleo Kwa familia zao.
Naye Bi.Miriam Ndakaji mkazi wa kijiji cha Engorika amesema "wanawake wengi Kwa sasa tumeamka katika kujishughulisha katika shughuli zinazotuinua kiuchumi na hata nafasi za uongozi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tumegombea nafasi mbalimbali na tumepata kwa asilimia kubwa ,hivyo nafasi ya mwanamke na kazi anazofanya kwa kipindi hiki huwezi kulinganisha na kipindi cha nyuma kwani tulikuwa tukidharaulika hatuchagui viongozi, hatupewi nafasi ya kuhudhuria vikao,sasa tumeelimishwa tukaekimika. "
Kwa upande wake Laigwanani Pelo Saning'o kutoka kijiji cha Lengloriti amepongeza jitihata zinazofanyika katika kuandaa midahalo mbalimbali, semina na UN WOMEN katika kuelimisha wanawake kwani wanawake wameendelea hasa katika sekta ya uongozi wengi ni wanawake,sio kama zamani ambapo wanawake awaruhusiwi kushika nafasi za uongozi.
Emmanuel zagila ambaye ni Mwalimu wa shule ya msingi Lengloriti ameeleza nikwanamna gani wanawake wameendelea hasa katika sekta ya Elimu ambapo watoto wa kike wamekuwa wakifanya vizuri darasani kuliko watoto wa kiume hivyo Kwa kipindi cha nyuma msichana alikuwa akibaki nyumbani na kufanya Shughuli za nyumbani.
Bi.Aimosaria Minja amehitimisha Kwa kuwapongeza wakina mama wa kata ya Naalarami Kwa tathmini ya matokeo mazuri katika kujitokeza kugombea nafasi za uongozi.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli