MBUNGE WA MONDULI FREDERICK LOWASSA AKABIDHIWA GARI YA AMBULANCE NA DC NASSARI KWENDA KITUO CHA AFYA NAFCO.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika hospitali ya Wilaya ya monduli tarehe 6.3.2024 ambapo Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Joshua Nassari amemkabidhi Mhe.Mbunge wa Jimbo la Monduli Frederick Lowassa gari hiyo na kuelekea Kituo cha afya Nafco kuwakabidhi wananchi wa wa kijiji cha Nafco kata ya Lolkisale.
"Mhe.Mbunge Fredrick Lowassa ni mtu wa vitendo zaidi kuliko maneno tunamshukuru sana kwakutusimamia maendeleo yawanamonduli kwani monduli ni ya vitendo na sio maneno"amesema katibu wa CCM Rukia Mbasha.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Monduli mhe.Fredrick lowassa amesema hakuna wilaya ambayo imepata bahati ya kupewa ambulance mbili kama wilaya yetu,hivyo ni vyema tutunze vizuri magari haya ya dharura kwa faida ya wananchi wa Monduli.
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi.Rose Mhina amesisitiza uweledi wa madereva katika uendeshaji wa magari hayo utumike kwaajili ya kutunza rasilimali zetu tunazoletewa na Serikali ya awamu ya sita.hivyo umakini wa madereva uangaliwe vizuri katika uendeshaji wa magari hayo.
"Tusiposhukuru kwa kidogo atuezi kushukuru kwa kikubwa kiukweli Serikali ya Mhe.Dtk Samia Suluhu Hassan imetuangalia sana sisi wananchi na wakazi wa monduli hivyo tunamshukuru kwa makubwa tunayotendewa magari matatu ndani miezi kadhaa katika Wilaya yetu na sio tu magari pamoja na vifaa tiba,Sekta ya afya awamu hii tumepewa kipaumbele kiukweli tunamshukuru sana Mama"amesema Nassari.
Makamu mwenyekiti halmashauri ya. Wilaya Monduli bwan.Thomas Meiyan ameshukuru kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri kwamba sisi tuliopata bahati kubwa hii ya kupata ambulance mbili hatuna budi kuzitunza kwa makini kwani zipo wilaya nyingi lakini sisi tumependelewa.
Hitimisho,Gari hiyo ya dharura (ambulance) Imekabidhiwa kwa Wananchi wa kijiji cha Nafco katika kituo cha afya Nafco kata ya Lolkisale na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Fredrick Lowassa.wananchi wa kijiji hicho wamepokea gari hiyo nakushukuru nakuaidi kuitunza na kuilinda kwani wamepata bahati kubwa hivyo wagojwa wa dharura watapata msaada kwa wakati.
Imeandaliwa na,
Kitengo cha mawasiliano serikalini
Halmashauri ya wilaya ya Monduli
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli