Mamlaka za Ukusanyaji wa fedha na mapato za Halmashauri na Mamlaka ya Mapato Wilaya ya Monduli zimatakiwa kutengeneza mahusiano mazuri na Wafanya Biashara ili kukuza na kuinua Hali ya Biashara katika Wilaya.
Wito huo Umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe Joshua Nassari akizungumza katika kikao cha Baraza la Wafanya Biashara kilichoketi katika ukumbi wa Halmashauri na kujadili hali ya Biashara kwa Wilaya ikiwemo Changamoto na mafanikio .
Mkuu wa wilaya amesema Kujenga Uadui kati ya Wafanya Biashara na Mamlaka za mapato na ukusanyi fedha ndio chanzo kikubwa cha kudorora kwa hali ya Biashara katika Wilaya, Hivyo kuwataka kudumisha mahusiano baina yao kwa kujali Lugha wanazitumia pamoja na kufanyia kazi Maoni ya Wafanya Biashara.
Kwa upande wao wafanyabishara Wamemshukuru mkuu wa Wilaya kwa Kusikiliza kero na maoni yao katika kikao hicho na kumuomba kuzifanyia kazi kwa Wakati ili kufanikisha Malengo ya wafanya Biashara hao.
Miongoni mwa Changamoto zilizotajwa na Wafanya Biashara hao ni pamoja na mahusiano hafifu kati yao watu wa Halmashauri, Changamoto ya mfumo wa Mpya wa ukusanyaji mapato TAUSI, Mwingiliano wa Wafanyabishara wa Vinyago katika Soko la mto wa mbu na Machinga wadogo.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli