Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Idd Hassan Kimanta pamoja na mbunge wa jimbo la Monduli Mhe. Julius Kalanga wamezindua machinjio ya kisasa katika kata ya Makuyuni wilayani Monduli. Uzinduzi huu ulifanyika mwishoni mwa mwezi desemba 2018. Machinjio haya yako eneo la shamba la manyara Ranch.
Ni nini hasa wasifu wa Manyara Ranch?
Ranchi ya manyara ina eneo lenye ukubwa wa hekta 17,800 na liko kwenye ushoroba wa wanyama pori unaounganisha Hifadhi za Taifa za Tarangire na Ziwa Manyara. Mwaka 2000, Ranchi ya Manyara ilibinafsishwa kutoka kwenye usimamizi wa Kampuni za Ranchi za Taifa (NARCO) na kukabidhiwa kwa Tanzania Land Conservation Trust (TLCT), ikiwezeshwa na AWF. TLCT ni chombo kilichoundwa kwa ajili ya kusimamia na kuendesha shughuli zote ndani ya Manyara Ranch. TLCT inajumuisha Vijiji vya Oltukai na Esilalei ambavyo ndivyo vyenye dhamana ya kusimamia na kuendesha shughuli za ufugaji pamoja na hifadhi ya ushoroba wa wanyama pori. Aidha eneo lililotengwa kwa ajili ya shughuli za Machinjio ni hecta 10 tu.
Ni nani anamiliki Machinjio hayo kwa sasa?
Kwa sasa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ndiyo yenye dhamana na usimamizi wa machinjio hii baada ya Serikali kuhuisha Hati ya umiliki wa Shamba la Manyara Ranch kutoka kwa Tanzania Land conservation Trust (TLCT) kwenda kwa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kwa manufaa ya Vijiji vya Oltukai na Esilalei.
Je machinjio hiyo imejengwa kwa shilingi ngapi?
Ujenzi wa jengo la Machinjio ya Makuyuni ulianza mwaka 2009 na hadi sasa haujamalizika. Gharama ya ujenzi wa jengo hili umeshagharimu jumla ya shilingi za Tanzania Shs.448,914,882/=.kwa mchanganuo ufuatao, ujenzi wa jengo la machinjio ni Tsh. 223,514,882 na ununuzi wa Mashine na vifaa vingine kwa ajili ya Machinjio viligharimu jumla ya Tshs.225,400,000/=.Ujenzi huu uligharamiwa na mtaji wa fedha (grant) kutoka USAID kupitia shirika la African Wildlife Foundation (AWF).
Kuanzia mwaka 2010 utaratibu uliandaliwa wa kuendesha machinjio hii ya Kisasa ikiwa ni pamoja na juhudi za kufanya mchakato wa kumpata mwekezaji atakayekodisha Machinjio hii, ili aweze kuingia mkataba na Halmashauri ya Wilaya ya Monduli na kuanza kazi ya uzalishaji. Tangu kipindi hicho (2010 hadi 2017)Tenda ilitangazwa lakini hadi sasa bado hajapatikana mwekezaji ambae ameonesha dhamira/nia ya kuwekeza.
Je, halmashuri ina mpango Mpango gani wa baadae, baada ya machinjio kukamilika?
Mpango wa baadae wa Machinjio hii ni Pamoja na kupanua wigo wa vyanzo vya mapato yanayotokana na kuuza mifugo na nyama iliyo bora katika kiwanda hicho, kutoza ushuru wa pango kutoka kwa mwekezaji atakaefanikiwa kuendesha kiwanda hicho. Sambamba na hilo kiwanda kitatoa soko la kuuza mifugo na nyama katika Vijiji vinavyozunguuka Machinjio.Pia itatoa ajira kwa wananchi ikiweka kipaumbele kwa jamii zilizo jirani na machinjio hiyo.
Je, kuna Changamoto zozote zinazosababisha machinjio yasifanye kazi kwa ufanisi?.
Zifuatazo ni changamoto/mapungufu yanayosababisha machinjio kutofanya kazi kwa ufanisi wake.
Ni mikakati gani iliyowekwa ya kukabiliana na changamoto hizo?
Asanteni; Nawatakia kheri ya mwaka mpya 2019.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli