Kamati ya Siasa ikiongozwa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Ndugu Rukia Mbasha imetembelea na kukagua baadhi ya Miradi ya utekelezaji katika Halmashauri ya wilaya ya Monduli.
Miongoni mwa Miradi waliyoitembelea ni pamoja na Jengo jipya la utawala la Halmashauri ya wilaya ya Monduli, Majengo mawili ya hospital ikiwa ni jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) pamoja na Jengo la Maabara pia Wametembelea Eneo la Dampo la Halmashauri lilipo kata ya Meserani.
Pia kamati imetembelea Shule mpya ya Sekondari Meserani pamoja na chuo cha ufundi Veta monduli kilichopo Kata ya Makuyuni, Wametembelea Mradi wa maji kata ya Esilalei pamoja na barabara kiwango cha lami latika kata ya Mto wa Mbu.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli