Kamati ya fedha na mipango Halmashauri ya wilaya ya Monduli imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika kata sita (6) Wilayani Monduli tarehe 29/1/2024.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya monduli Ndug.Isack Copriano , Kwakuanza na kutembelea ujenzi wa matundu ya vyoo shule ya msingi Sinoni ametoa maelekezo kwa wajumbe na Afisa Elimu Msingi Bi.Natang'aduak Mollel kusimamia kusimamia vizuri fedha ambazo serikali imepeleka kwaajili ya ujenzi huo kukamilika kwani kwa kiwango cha fedha kilichotumika na sehemu iliyobakia kukamilisha ujenzi avilandani na salio la pesa lililobakia.
"Wakati mwingine tubane na tufinye pesa za serikali kwa kutumia vizuri na kwakuona ile pesa ni ya kwako ili kueza kumalizia ujenzi wa matundu ya vyoo"amesema Isack.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa kamati ya fedha, atoa maelekezo kwa shule ya sekondari Mswakini avunja kamati ya ujenzi na kuagiza kamati nyingine kuudwa ili kueza kukamilisha ujenzi wa bweni la wanafunzi.
Akizungumza na wajumbe wa kamati ya fedha amesema ni milioni 138,205,154 Tsh.Fedha ambazo mhe.Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ameleta Mswakini Sekondari kwa ajili ya kuwajengea mabweni haya hivyo tusicheze na fedha hizo kwa matumizi yasiyo stahiki kama vile walivyofanya kwenye ununuzi wa kokoto za kuanzia kujenga kwani sio matumizi mazuri amemsisitiza afisa Elimu Sekondari kusimamia kwa umakini.
Vivyo hivyo,kata ya Mingungani kwenye ziara yake ametoa maelekezo ya marekebisho ya ujenzi ya nyumba ya walimu 2 in 1 waakikishe waalimu wanahamia mara baada ya marekebisho kufanyika kama vile kupiga msasa madirisha yote.ndipo waahamie.
Hitimisho kamati ya fedha uongozi na mipango wamepongeza kata ya Selela,Shule ya Sekondari Oltinga kwa ujenzi wa madarasa mawili pamoja na ujenzi wa matundu ya vyoo.nakuaidi kwamba zitatafutwa fedha kwaajili ya kumalizia ujenzi wa mabweni.
Imeandaliwa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serekalini
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli