Jeshi la wananchi Tanzania -JWTZ wa shule ya mizinga (School Of Artillery) - SOFA katika kuazimisha siku ya mashujaa Tanzania leo tarehe 25/07/2018, wamefanya usafi katika hospitali ya wilaya ya Monduli. Wanajeshi hao wakiongozwa na Mkuu wa shule hiyo wamefanya usafi katika maeneo yote ya ya hospitali hasa katika eneo la kuzunguka wodi za wagonjwa. Kazi zilizofanyika ni pamoja na kufyeka nyasi ndefu, kutengenezea bustani za maua, kuchoma taka na kuchimba mashimo ya taka.
|
Mkuu wa SOFA kanali Mosses Gambos alisema kuwa wao wameamua kufanya uzalendo kwani jeshi ni sehemu ya jamii na ni jeshi la wanachi, pia kwa upande mwingine ni wajibu wao kufanya shughuli za kijamii wakati wa amani. Pia Gambos ametoa wito kwa wananchi wengine kujitolea kufanya shughuli za kijamii kama wao waliyojitolea.
Mganga Mkuu wa wilaya ya Monduli Dr. Titus Mmasi wakati akitoa pongezi na shukrani amesema, anashukuru kwani si mara ya kwanza kwa wanajeshi hao kufanya kazi hiyo ambayo wadau wengine ni mara chache kuifanya. Pia katika kuchangia damu na kwenye kampeni za matibabu wamekuwa mstari wa mbele kujitolea na kuhamasisha.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli