Msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Monduli Ndugu; Steven Anderson Ulaya ametangaza matokeo ya marudio ya uchaguzi wa ubunge wa jimbo la Monduli kama ifuatavyo.
Elizabeth Michael Salewa (Chama cha Wakulima) kura 16 Sawa na 0%, Wilfred Willium Mlay (ACT wazalendo) kura 144 Sawa na 0%, Francis Silas Ringo (ADA-TADEA) kura 21 sawa na 0%, Julius Kalanga Laizer (CCM) kura 65704 Sawa na 95%, Yonas Masiaya Laiser (CHADEMA) kura 3187 Sawa na 5%, Omary Mwenjuma Kawaga(DP) kura 34 sawa na 0%, Simon Paulo Ngilisho (MAKINI) kura 35 sawa na 0% na Feruziy Juma Feruziyson(NRA) kura 45 sawa na 0%.
Kwa matokeo haya Julius Kalanga Laizer wa chama cha mapinduzi (CCM) ametangazwa tena mbunge wa jimbo la Monduli. Julius Kalanga alihama CHADEMA na kujiunga na CCM mwanzoni mwa mwezi wa saba mwaka 2018, hivyo kusababisha kufanyika upya kwa uchaguzi. Kalanga aliteuliwa tena na CCM kugombea ubunge ambapo ameibuka mshindi na kutunukiwa cheti cha ushindi na msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Monduli.
Uchaguzi huu ulifanyika tarehe 16/9/2018 siku ya jumapili na matokeo kutangazwa saa tano usiku.
E.Msifuni
A/TEHAMA
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli