HALMASHAURI YA WILAYA YA MONDULI YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE YA KIWILAYA KATA YA SELELA.
Maadhimisho hayo yaliyoambatana na kauli mbiu isemayo"wekeza kwa wanawake kuharakisha maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii" yamefanyika katika kata ya selela ambapo Mhe.Diwani kata ya Selela Richard Ndoroso amemwakilisha Mgeni rasmi kweye hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya wanawake Selela.
Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni maendeleo ya jamii Bi.Rose mhina Amewapongeza wanawake kujitokeza kwa wingi wao kwenye hafla hiyo.lakini pia ametoa nafasi kwa wanawake wote kupewa elimu ya masuala mtambuka.Haki za kumiliki ardhi kwa wanawake.pamoja na kumuinua mwanamke kiuchumi.
Vivyo hivyo pia wadau mbali mbali wamepata nafasi yakutoa elimu siku ya wanawake na wananchi kama Mratibu wa mama na mtoto,polisi jamii,afisa mipango miji na vijiji,PWC,sinoni ngarash,CORDS na wengine wengi.
"Swala la elimu kwa akina mama liendelee kupewa kipaumbele kwani ukimuelimisha mwanamke mmoja umeielemisha jamii lakini pia wakina mama ni jeshi kubwa sio kwa ufanyaji wa biasha na hata maendeleo ya jamii kwa ujumla nawapongeza sana wanawake"amesema mhe.Diwani kata ya Selela Richard.
Halikadhalika,Shirika la Ujamaa Community Resources Team (UCRT) Shirika lisilo la kiserikali katika wilaya mbalimbali ikiwepo Wilaya ya Monduli kwa kuthamini siku ya wanawake duniani na kutambua jitihada kubwa za mwanamke kwa kugawa Hati miliki za kimila (CCRO)zipatazo 150 zenye gharama ya sh.milion saba na laki tano (7,500,000) kwa makundi yafuatayo (wamama,vijana na walemavu)kutoka kata ya Engaruka.pamoja na kuwagaia mbuzi 40 zenye thamani ya sh.4000000 milioni nne.
Hitimisho Mhe.Diwani Napir mukere Tarafa ya manyara kata ya Selela amewashukuru wanawake kwa umoja wao kuhudhuria katika hafla ya siku ya maadhimisho hayo ya wanawake ambapo pia amesema kuwa mwanamke ni jeahi kubwa na mwenye uwezo wakujikwamua kiuchumi na pia leo kwasababu wanawake wengi wapo katika biashara ikiwa ni siku ya soko Selela wengi wao hawapo lakini kwa jeshi letu kubwa hili tunashukuru kwa mahudhurio naimani kila mmoja amepata kitu katika siku hii.
Imeandaliwa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serekalini
Halmashauri ya Wilaya Monduli
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli