Na Mwandishi wetu
Obed Emmanuel.
Jamii imetakiwa kuwalea watoto katika malezi bora kwa kuwapatia elimu ili kuunga mkono juhudi za Mhe Raisa wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Samia suluhu Hassan za kuiendeleza sekta ya elimu nchini.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe Joshua Nasary katika kikao kazi cha kutadhmini na kumpongeza Juhudi za wadau wa elimu kwa mwaka 2022 kilicho fanyika katika ukumbi wa chuo cha maendeleo ya Jamii CDTI monduli.
Mhe. Nasari amesema katika karne hii ya 21 ni ajabu sana kuona au kusikia mzazi anamuodhesha binti badala ya kumpeleka shule katika kipindi hiki ambacho Rais ameruhusu elimu bure.
Aidha amesema ni ni jukumu la wazazi pamoja na wadau hao wa elimu kushirikiana kulea Watoto katika mazingira bora na kuwapatia elimu itakayo wasaidia katika maisha ya kila siku.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli Mhe Isack Copriano pia amewapongeza walimu wakuu wote wa wilaya ya Monduli kwa kuendelea kufanya kazi kwa ueledi na umakini ili kuendelea kutokomeza daraja sifuri katika wilaya nzima ya Monduli.
Nae Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli Mhe. Thomas Meiyan Amesema ili kufanikisha ndoto za wilaya na katika elimu ni lazima wazazi/walezi washirikiane katika malezi bora ya watoto wawepo washulenj au nyumbani.
Awali Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Monduli Bi Magreth Muro Akisoma taarifa kwa mgeni rasmi amesema kwa mwaka 2022 wamefanikiwa kuongeza ufaulu kwa shule za sekondari na wanatajia kufikia 99% kwa mwaka 2023.
Wadau wa elimu, walimu pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri katika mitiani kwa mwaka 2022 wamepokea zawadi za pongezi ikiwa ni sehemu ya kuwatia motisha ilinwaendelee kufanya vizuri zaidi.
Ofisi ya Tehama
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli