Mhe. Festo S. Kiswaga Mkuu wa wilaya ya Monduli Leo Septemba 10, 2024 amefanya kikao na watumishi wa Idara ya Afya wa Hospitali ya Wilaya ya Monduli chenye lengo la kuwakumbusha wajibu na majukumu yao ya kazi ambayo kwayo Serikali imewaamini na kuwaajiri ili wawahudumie Wananchi kiafya Kwa maendeleo ya Taifa letu.
" Nimeona tuzungumze kama familiya Kwa kuwa sisi sote tunafanya kazi za kuwahudumia Wananchi wa Wilaya yetu ili tuwekane sawa na tutoe Huduma nzuri Kwa Wateja wetu. Na kwakuwa ninyi mmeaminiwa na Serikali mnapaswa kutoa Huduma kwa haki na kwa wakati. " Amesema Mhe. Kiswaga
Akizungumza na watumishi hao wa afya Mhe. Kiswaga amesema kutokana na uwepo wa malalamiko mengi anayoyapokea kutoka kwa Wananchi, imeomekana dhahiri kuwa utendaji kazi wa watumishi hospitalini hapo si mzuri jambo linalopelekea wananchi kulalamika ya kwamba wanapoteza muda mwingi kusubiria kupata huduma jambo linalochelewesha watu kupona na kuendelea na shughuli za maendeleo.
Mhe. Kiswaga ameongeza kuwa wagonjwa wanakaa muda mrefu bila kupata huduma kwani watoa huduma wanakuwa hawapo Katika maeneo yao ya kazi (ofisini) wakazi wa kazi.Amemtaka Mganga Mkuu huyo kumwandikia taarifa inayo onyesha ni wapi wagonjwa hao wanacheleweshwa kupata huduma mara wanapofika hospitalini hapo.
Sambamba na hayo Mhe. Kiswaga amebaini kuwa wapo watumishi ambao wamekuwepo Katika eneo hilo la kazi (Hospitali ya Wilaya ya Monduli) Kwa miaka zaidi ya 20 jambo ambalo amewataka wasizoelee kazi Wala mazingira bali watumie fursa hiyo na weledi walionao kufanya kazi kwa ufasaha na ufanisi mkubwa.
Aidha, Mhe. Kiswaga amemtaka Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dr. George Kasibante kuandaa mafunzo ya siku mbili ndani ya wiki mbili zijazo ili watumishi wote wa afya hospitalini hapo wakumbushwe na kufundishwa juu ya suala la huduma Kwa Wateja hatimaye wajitambue na kukumbuka wajibu wao Kwa Wananchi wanao wahudumia, na katika mafunzo hayo ameahidi kuwa Mgeni rasmi atakae yafungua.
Ameongeza kuwa baada ya mafunzo hayo sitegemei tena Mganga Mkuu awakumbushe kila siku wajibu wenu wa kuwahudumia wananchi bali Kila mmoja wenu ajitambue na kujuwa ni nini anapaswa akifanye kwa manufaa ya Wananchi.
Naye Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dr. George Kasibante amejibu hoja hiyo Kwa kusema Katika maeneo yote anakopitia Mgonjwa ukianzia mapokezi sehemu pekee anakoweza kutumia muda mrefu ni maabara ambako vipimo vya muda mrefu zaidi ni muda wa saa moja (1).
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Wilaya ya Monduli Bi. Happiness Laizer amemshukuru Mkuu wa wilaya Mhe. Kiswaga Kwa kuwakumbusha watumishi wa Idara ya afya Wilayani hapo wajibu wao na ameahidi kuwa mafunzo aliyoagiza yatafanyika Kwa wakati. Pia kamshukuru Mhe. Kiswaga kuwa bega Kwa bega Katika kuhakikisha ujenzi wa majengo ya OPD,ufuaji, Mionzi na jengo la upssuaji yanakamilika Kwa wakati.
Mhe. Kiswaga amewasisitiza watumishi hao wa Idara ya Afya kuwa "umeajiriwa kama mtumishi na hii si kazi ya familiya Wala si eneo la biashara Dr. Samia Suluhu Hassan ametoa pesa nyingi ili kuhakikisha mazingira ya kazi yanaboreshwa yaani majengo, vifaa tiba na madawa hivyo si vema mwananchi kucheleweshwa anapohitaji Huduma."
Mhe. Festo Kiswaga amehitimisha kwa kumpa mwezi mmoja Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Monduli kuruhusu majengo ya OPD, Mionzi, upasuaji na ufuaji kuanza kutumika kuanzia Oktoba 10, 2024.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli