Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Festo Kiswaga ameagiza jamii kuzingatia umuhimu wa lishe Bora kwa watoto ili kuepukana na udumavu.
Kiswaga ametoa rai hiyo Novemba,8 2024 wakati wa maadhimisho ya Lishe ngazi ya wilaya yaliyofanyika kata ya Migungani katika Halmashauri ya Monduli.
Amesema kuwa suala la lishe bora ni muhimu kwa jamii kuendelea kuzingatia kwani ili kuwa na Familia Bora na Taifa bora ni lazima lishe ipewe kipaumbele kwa watoto kwa kuwa watoto wenye lishe bora hata uwezo wao wa kiakili huwa mkubwa.
serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa Mbele kuhamasisha lishe Bora na ni vema Kila mmoja kuweka mkazo wa lishe bora kwa watoto .
Pia Kiswaga amewataka wanawake wenye watoto wanaonyonya kuzingatia unyonyeshaji mzuri wa watoto kwa kwani kunyonyesha maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya mwanzo pamoja na matumizi ya vidonge vya kuongeza damu kwa wajawazito iwe kipaumbele .
Ameeleza kuwa lengo la maadhimisho haya ni kutoa elimu kuhusu lishe bora na kuhamasisha jamii ili kuepuka magonjwa yanayotokana na lishe duni kama vile kisukari, shinikizo la damu, utapiamlo, na upungufu wa damu kwa wajawazito na watoto wachanga.
Hivyo aliitaka jamii kuchangia chakula kwa watoto mashuleni, kuanzisha klabu za lishe mashuleni, na kutumia vyakula vilivyorutubishwa kwa madini na vitamini muhimu.
"Lengo likiwa ni kuboresha afya na lishe ya watoto, vijana balehe, wajawazito, wanaonyonyesha, wazee, na jamii kwa ujumla"
Kwa upande wake,Mganga mkuu wa Wilaya, Dkt. George Kasbante, amesema kuwa lishe bora ni muhimu kwa wakazi wa Kata ya Migungani na Wilaya nzima kwa ujumla hivyo ni vyema kuangalia hali zetu za kwa kuzingatia milo kamili.
Afisa Lishe wa Wilaya, Michael Mhombo amezitaja changamoto kubwa kuwa ni tabia ya baadhi ya wananchi kula vyakula ambavyo si mchanganyiko na vina upungufu wa virutubishi. Kama virutubishi vinavyopatikana kwenye matunda, mbogamboga, na mazao ya wanyama kuwa tabia hiyo husababisha hatari ya utapiamlo na magonjwa sugu yasiyoambukiza, na kupelekea ongezeko la wajawazito wenye upungufu wa damu.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli