Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Festo S. Kiswaga ametoa shukrani za dhati Kwa Benki ya NMB kuendelea kuwa wadau pekee Katika wilaya ya Monduli ambao siku zote wamekuwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano wa hali na Mali Katika kutoa msaada pale msaada unapohitajika.
Mhe. Kiswaga ameyasema hayo Leo Septemba 11, 2024 wakati akipokea msaada wa vifaa tiba Kwa ajili ya kuboresha huduma za Afya Katika Hospitali ya Wilaya ya Monduli vyenye thamani ya shilingi milioni 6.5.Vifaa hivyo ni pamoja na:- Vitanda vitano(5),. Magodoro matano(5), Mashuka mia moja(100), Drip stand Tano (5),Vitanda vya uchunguzi ( examination bed) tatu (3),Vitanda vya magurudumu (wheelchair) vitatu (3).
Akipokea vifaa hivyo kutoka kwa Bi. Vicky Bishubo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Biashara NMB. Mhe. Kiswaga amesema " Benki ya NMB mme kuwa wadau wakuu katika kumuunga mkono Rais wetu makini Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusimama upatikanaji huduma bora za Afya na kuboresha mazingira ya utoaji huduma hizi mjini na vijijini. Hivyo vifaa hivi vitasaidia utoaji na upatikanaji wa huduma nzuri na kuwawezesha wagonjwa wanaohudumiwa hospitalini hapo kutibiwa Katika mazingira bora. "
Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Monduli Dkt. George Kasibante amemshukuru Benki ya NMB kwa kutoa vifaa tiba hivyo ambavyo vitaongeza ufanisi Katika kuboresha utendaji kazi na utoaji huduma Kwa wagonjwa. Ameongeza kusema kuwa Kwa uwepo wa vifaa hivi tunatarajia kutoa Huduma kwa wagonjwa kuanzia 80 hadi 120 Kwa siku.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mhe. Isack Copriano amewapongeza Benki ya NMB tawi la Monduli na kusema " Jambo hili mlilolifanya ni la Ki- Mungu kwani kile kidogo mnacho kupata kama faida kutoka kwa wateja mmeona mkigawanye na kukirudisha kwa wananchi. Hii inaonesha namna ambavyo benki ya NMB inavyowajali wananchi wa Monduli.
Aidha, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Happiness R. Laizer amemshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Halmashauri ya Wilaya ya Monduli fedha za ujenzi wa majengo ya OPD, Mionzi, upasuaji na ufuaji. Pia ameishukuru Benk ya NMB Kwa kuendelea kuwa na mahusiano mazuri na Wilaya ya Monduli "pamoja na kwamba mme kuwa mkitupatia msaada wa madawati Kwa shule zetu bado mko pamoja nasi na sasa tumeshuhudia mkitupatia vifaa tiba ambavyo vitapelekea Wananchi wetu kupata huduma nzuri. Kwa kweli Kwa hili mmeigusa jamii moja Kwa moja." Amesema Bi. Happiness Laizer
Akihitimisha mapokezi ya vifaa hivyo, Mhe. Kiswaga amewataka wana Monduli kujenga tabia ya kuja kwenye hospitali yetu hii kupima hata kama hawaumwi ili kuepuka gharama kubwa ambazo yamkini wangezipata kama wangekuja kutibiwa wakiwa wagonjwa. Pia amemsisitiza Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo kuvitumia na kuvihifadhi vifaa hivyo kwa umakini ili viweze kutumika kwa muda mrefu kwa manufaa ya Wana Monduli na watanzania kwa ujumla.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli